Lugha Nyingine
Kampuni ya China yakabidhi msaada wa vifaa vya kazi nzito kuboresha barabara nchini Ghana
Kampuni ya utengenezaji wa mitambo mikubwa ya China LiuGong, imekabidhi vifaa zaidi ya 2,200 vya kazi nzito kwa serikali ya Ghana kuunga mkono Mpango wa Uboreshaji wa Barabara za Wilaya nchini Ghana (DRlP).
Vifaa hivyo ni pamoja na magreda, matingatinga, mashine za kuchanganya zege, mashine za kushindilia, malori ya kubeba mchanga na maboza, vilivyonunuliwa na serikali ya Ghana kwa ajili ya ukarabati wa barabara.
Wakati wa hafla ya makabidhiano Rais Nana Akufo-Addo amesema mradi huo unaashiria hatua muhimu katika harakati za Ghana za maendeleo ya miundombinu. Pia amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana katika maendeleo ya nchi, barabara nyingi, hasa katika wilaya zisizo na uwezo, bado ziko katika hali isiyo ya kuridhisha, na kukwamisha shughuli za kiuchumi na juhudi za maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma