Lugha Nyingine
Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Zambia
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Zambia Bw. Mulambo Haimbe jana Jamatano hapa Beijing.
Bw. Wang Yi amesema, China inaishukuru Zambia kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China-Moja na iko tayari kuimarisha msingi wa kuaminiana, kuzidisha ushirikiano wenye matokeo halisi, na kuendelea kuungana mkono na Zambia katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya kila mmoja wao.
Bw. Wang ametoa wito kwa pande mbili kuimarisha na kuhuisha kwa pamoja Reli ya TAZARA, kuratibu maendeleo jumuishi ya maeneo yaliyoko karibu na reli hiyo, kuisaidia Zambia kubadilisha raslimali zake kuwa msukumo wa maendeleo, na kuinua uwezo wake wa kujiendeleza na kiwango chake cha maendeleo ya viwanda.
Kwa upande wake Bw. Haimbe amesema Zambia inapenda kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yake na China, kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma