超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Wataalamu wakutana nchini Kenya ili kuoanisha viwango vya bidhaa barani Afrika

(CRI Online) Agosti 02, 2024

Wataalamu wa Afrika wanakutana huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya kuanzia siku ya Alhamisi kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Mfumo wa Metrolojia wa Afrika na Mkutano wa Kiufundi, ili kujadili kuhusu njia za kuoanisha viwango vya bidhaa barani humo.

Mkutano huo ulioanza Alhamis na umepangwa kuendelea kwa siku tano, umewaleta pamoja maofisa wa Umoja wa Afrika na mamlaka za udhibiti wa ubora wa viwango kutoka kote barani ili kuhimiza maendeleo ya kuoanisha viwango vya bidhaa.

Katibu Mkuu wa wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda ya Kenya Bw. Juma Mukhwana amesema, moja kati ya sababu za biashara barani Afrika kuwa ya chini ni ukosefu wa kutambuana viwango vya biadhaa kati ya serikali za nchi mbalimbali barani Afrika.

Amesema, viwango vinavyofanana vitapunguza vikwazo visivyo vya kiushuru kwa bidhaa zinazotengenezwa katika nchi moja ya Afrika na kuuzwa katika nchi nyingine.

Amebainisha kuwa jumuiya za kiuchumi ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki zitaharakisha kufikiwa kwa viwango vya pamoja vya bidhaa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha