Lugha Nyingine
Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini waunganisha bandari 523 duniani
Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini waunganisha bandari 523 duniani kote
CHONGQING - Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini umefikia bandari 523 katika nchi na maeneo 124 huku ukiwa na kituo chake cha uendeshaji katika mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, ukanda huo unaunganisha bandari za kimataifa kupitia reli, njia za baharini na barabara kuu kupitia mikoa ya kusini mwa China kama vile Guangxi na Yunnan.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Jumatatu na kituo cha uratibu wa uchukuzi na uendeshaji cha Ukanda huo, treni zaidi ya 30,000 za mizigo kati ya China na Ulaya zimefanya kazi kupitia ukanda huo wa kibiashara.
Kuanzia Mwaka 2019 hadi Mwaka 2023, kiasi cha mizigo kupitia ukanda huo kutoka Chongqing cha kila mwaka kiliongezeka kwa asilimia 50, asilimia 45, asilimia 54, asilimia 32 na asilimia 21 mtawalia.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, aina mbalimbali za bidhaa zinazosafirishwa kupitia ukanda huo zimepanuka kutoka aina zaidi ya 80 hadi aina zaidi ya 1,150, zikijumuisha bidhaa za kielektroniki, magari na vipuri vyake, mashine, vifaa vidogo vya matumizi ya nyumbani na chakula. Ukanda huo wa biashara sasa umepata uwiano wa karibu kati ya usafirishaji bidhaa zinazoingia na zinazotoka.
Kwa kutegemea ukanda huo wenye kasi ya haraka na ufanisi, bidhaa maarufu kutoka magharibi mwa China, kama vile juisi ya goji berry na divai nyekundu kutoka Ningxia, machungwa kutoka Chongqing na chai kutoka Guizhou, zimekuwa vichocheo vipya vya ukuaji wa biashara ya kuuza bidhaa nje.
Zaidi ya hayo, uuzaji wa magari yanayotumia nishati mpya kutoka mikoa hiyo ya magharibi umeongezeka, huku kampuni za magari za mikoa hiyo zikianzisha viwanda katika nchi za Asia Kusini-Mashariki.
Wakati huo huo, bidhaa maalum za Asia Kusini-Mashariki kama vile doriani za Thai na samaki wa basa wa Vietnamese zinaingia kwenye soko la China kwa haraka zaidi kupitia ukanda huo.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma