Lugha Nyingine
Chebet wa Kenya ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2024
Mkenya Beatrice Chebet alifanya umalizaji wa kishindo ili kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000 kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alivuka mstari wa mwisho wa mbio hizo kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 28.56, zaidi ya sekunde mbili mbele ya bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi, ambaye amepata medali ya fedha.
Nadia Battocletti wa Italia amepata medali ya shaba kwa kumaliza mbio kwa dakika 14 sekunde 31.64.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma