Lugha Nyingine
Siku ya 14 ya Michezo ya Olimpiki ya Paris: Timu ya tenisi ya mezani ya China yalinda ubingwa, Hispania yanyakua medali ya dhahabu ya soka (3)
Chen Yiwen wa China akishindana kwenye fainali ya kupiga mbizi kwa wanawake kutoka jukwaa la kimo cha mita 3 katika Michezo ya Olimipiki ya Paris Agosti 8, 2024. (Xinhua/Wang Peng) |
Timu ya tenisi ya mezani ya wanaume wa China ilidumisha ubingwa wake wa tano mfululizo wa Olimpiki baada ya kushinda timu ya Sweden kwa 3-0 katika Michezo ya Paris 2024 siku ya Ijumaa, na siku hiyo hiyo timu ya Hispania ilishinda Ufaransa kwa 5-3 na kunyakua medali ya dhahabu katika soka kwa wanaume.
Baada ya Siku ya 14, China na Marekani zimechukua nafasi ya kwanza katika jedwali la medali za dhahabu, kila moja ikiwa na dhahabu 33. Hata hivyo, Marekani inaongoza kwa medali za fedha, ikiwa na 39 ikilinganishwa na 27 za China.
Nyota wa kupiga mbizi wa China, Chen Yiwen aliongeza medali nyingine ya dhahabu. Alishinda shindano la kupiga mbizi kwa wanawake kutoka jukwaa la kimo cha mita 3, na kufikisha jumla ya medali saba za dhahabu kwa timu ya kupiga mbizi ya China katika Michezo hii.
Xu Shixiao na Sun Mengya wa China walilinda ubingwa wao katika mbio za mtumbwi za mita 500 kwa wanawake wawili. Walimaliza sekundi 1.49 mbele ya Liudmyla Luzan na Anastasiia Rybachok wa Ukraine.
Bondia wa China Wu Yu alipata medali ya dhahabu katika mchezo wa ndondi kwa mabondia wanawake wenye uzito wa kilo 50, akimshinda Buse Naz Cakiroglu wa Uturuki kwa alama 4-1. Ushindi huu ulileta medali ya pili ya dhahabu ya ndondi kwa China katika Paris 2024.
Mashindano ya riadha yaliendelea kung'ara. Canada ilipata dhahabu yao ya kwanza ya riadha kwenye Paris 2024 kwa kushinda mbio za wanaume za 4x100m. Andre De Grasse wa Canada alimzidi Akani Simbine wa Afrika Kusini katika mzunguko wa mwisho, na kuifanya timu yake imalize kwa sekundi 37.50.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma