Lugha Nyingine
Watu wa kizazi cha wavamizi wa Japan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia waomba msamaha kwa ukatili wa uvamizi na kutoa wito wa amani
CHANGCHUN - Chini ya bendera ya taifa la China, raia wa Japan mwenye umri wa miaka 76 Kuroi Akio amevua viatu na soksi zake na kupiga magoti kushujudu mbele ya watu wa China wakati alipoamua kuomba msamaha kwa niaba ya baba yake katika eneo la kihistoria lililoko Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, ambako vikosi vya Japan vilifanya ukatili wakati vikiivamia China.
Kabla ya siku ya kumbukumbu za Tukio la Septemba 18, Kuroi, pamoja na watu wengine wanane wa kizazi cha wanajeshi wa Japan walioivamia China, walianza safari ya siku tano ya majuto na kuomba msamaha.
Septemba 18, 1931, wanajeshi wa Japan walishambulia kambi kadhaa za kijeshi za China na kuanza uvamizi wa umwagaji damu nchini China, ulioashiria kuanza kwa vita vya pili vya dunia na kuifanya China kuwa ya kwanza kufanya mapambano dhidi ya ufashisti.
Jeshi la Japan lilikuwa limetuma wanajeshi milioni 1.86 nchini China, idadi ambayo ilikuwa zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya wanajeshi wote milioni 3.58 wa Japan waliotumwa ng'ambo.
Kwenye vita vya kupambana na uvamizi wa Japan vilivyodumu hadi Mwaka 1945, China ilipoteza wanajeshi na raia milioni 35, idadi ambayo inachukua theluthi ya jumla ya vifo vyote vya watu vilivyotokea katika nchi zote katika WWII.
Baba yake Kuroi, Kuroi Keijirou, alishiriki katika operesheni mbili tofauti kaskazini-mashariki mwa China mwaka 1932 na 1941. Operesheni hizo zilijumuisha vitendo vya kikatili dhidi ya raia, jambo ambalo Kuroi Akio amedhamiria kushughulikia na kulijutia kwa kuliombea msamaha.
Akitembea katika maeneo ya zamani yaliyokuwa yamekaliwa kijeshi na Japan, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya kamandi na kambi, Kuroi ametafakari juu ya maovu hayo ambayo kikosi cha baba yake kilisababisha.
"Walifanya mashambulizi dhidi ya wakulima na wakazi wa Mji wa Gongzhuling, wakiwadhulumu maisha yao na kuwapora mali zao. Vitendo vya baba yangu havikuwa vya kibinadamu, na nikiwa mtoto wake, natoa pole zangu za dhati kwa watu wa Gongzhuling. Alichokifanya hakiwezi kusameheka,” Kuroi amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma