Lugha Nyingine
Viongozi katika?UNGA waeleza wasiwasi mkubwa na ghasia za Mashariki ya Kati, waikosoa Israel kwa "mauaji ya halaiki"
UMOJA WA MATAIFA - Viongozi wanaohutubia Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) siku ya Jumanne wametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia ambazo zimekuwa zikiikumba Mashariki ya Kati kwa miezi kadhaa, na baadhi yao wamenyoosha vidole vyao moja kwa moja kwa Israeli kwa "mauaji ya halaiki" yanayofanywa dhidi ya Wapalestina.
Rais wa UNGA Philemon Yang amebainisha migogoro mbalimbali inayoendelea kuanzia Mashariki ya Kati hadi Ukraine, na kuanzia Haiti hadi Sudan Kusini. "Natoa wito wa kusimamishwa kwa mapigano mara moja katika mazingira haya yote ya migogoro," amesema, akiongeza kuwa watu wa Gaza na Israel "wamekamatwa katika mzunguko wa migogoro na ulipizaji kisasi" kwa karibu mwaka mmoja.
Akitoa ripoti yake ya mwaka 2024 kuhusu kazi ya Umoja wa Mataifa kabla ya Mjadala Mkuu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa viongozi wa dunia wanakusanyika katika kivuli cha migogoro inayoendelea Gaza, Ukraine, Sudan na kwingineko, na kuongezeka hali ya kutokuwa na uhakika juu ya mabadiliko ya tabianchi, kumaliza umaskini na kuchukua nafasi kwa akili mnemba.
"Dunia yetu iko katika kimbunga. Tuko katika zama za mageuzi makubwa -- tunakabiliwa na changamoto tofauti ambazo hatujawahi kuona -- changamoto zinazohitaji suluhu za kimataifa," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema taifa lake limenufaika kutokana na wimbi la mshikamano wa kimataifa katika vita vya kukomesha ubaguzi wa rangi na kuanzisha zama mpya ya kidemokrasia. "Hatutakaa kimya na kutazama wakati ubaguzi wa rangi ukifanywa dhidi ya wengine" huko Gaza wakati Israeli ikiendelea na adhabu yake ya ujumla kwa Wapalestina, ameongeza.
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameilaani Israel kwa "kupuuza haki za msingi za binadamu, kukanyaga sheria za kimataifa katika kila fursa, kutekeleza mauaji ya kikabila, mauaji ya halaiki ya wazi dhidi ya taifa na watu, na kukalia ardhi zao hatua kwa hatua."
Rais wa Mareakni Joe Biden amesisistiza juu ya umuhimu wa diplomasia katika kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati. Kwa kweli, inaendelea kuwa njia pekee ya usalama wa kudumu."
"Hilo ndilo tunalofanya kazi bila kuchoka ili kulifikia," Biden amesema.
"Tunapotazama mbele, ni lazima pia tushughulikie ongezeko la ghasia dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuweka mazingira ya mustakabali mzuri zaidi, ikiwa ni pamoja na suluhu ya mataifa mawili, ambapo Israel inafurahia usalama na amani na kutambuliwa kikamilifu, na kuweka hali ya kawaida ya uhusiano na majirani zake wote ambapo Wapalestina wanaishi kwa usalama, heshima na kujitawala katika taifa lao wenyewe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma