Lugha Nyingine
Watu Washerehekea Sikukuu ya Kijadi ya Chongyang pia Siku ya?Wazee ya China Katika Jumuiya ya Makazi
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2024
Wazee wakifanya onyesho la kucheza na kupiga ngoma ikiwa kiunoni kwenye kituo cha jumuiya ya makazi ya mtaa, Oktoba 10.(Xinhua/Weng Xinyang) |
Jumuiya ya makazi ya Jiangnan katika Mji wa Shengzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China ni jumuiya ya makazi ya ngazi ya mkoa ya siku za baadaye katika mkoa huo wa Zhejiang. Sikukuu ya Chongyang, ambayo pia huitwa Sikukuu ya Tarehe Tisa Mwezi wa Tisa kwa Kalenda ya Kilimo ya China au Siku ya Wazee ya China inapowadia, wazee wa jumuiya hiyo wameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za kupendeza katika sikukuu hiyo.
Jumuiya ya makazi ya siku za baadaye ni dhana ya jumuiya iliyopendekezwa na Mkoa wa Zhejiang. Inajikita katika mahitaji ya huduma katika mnyororo kamili wa maisha katika jumuiya za makazi ili kujenga ufanyaji kazi wa jumuiya za makazi mijini wenye teknolojia za kisasa na utulivu wa mwili zaidi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma