超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Binti mtoto wa Tanzania mwenye umri wa miaka 5 anafuata nyayo za baba yake akibobea?katika kung fu ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2024
Binti mtoto wa Tanzania mwenye umri wa miaka 5 anafuata nyayo za baba yake akibobea?katika kung fu ya China
Mariam Saidi Mfaume (wa pili kushoto), binti mtoto wa Tanzania mwenye umri wa miaka mitano, akifanya mazoezi ya kung fu ya China katika Klabu ya Kung Fu ya Hekalu la Shaolin ya Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Novemba 30, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Kwa Mariam Saidi Mfaume, binti mtoto wa Tanzania mwenye umri wa miaka mitano, mbingu pekee ndio ukomo wake anapoingia kwenye ulimwengu wa kung fu, sanaa ya kupigana ya Wachina, kama vile inavyokuwa kwa baba yake.

Siku za Jumamosi zenye jua kali, Mariam kwa kawaida anapata mafunzo kwenye Kiwanja cha Toangoma, Wilaya ya Temeke, umbali wa kilomita takriban 30 kusini mwa jiji la Dar es Salaam, ambako anafanya mazoezi ya kung fu na wenzake wengine 10.

"Shauku ya Mariam katika kung fu ilianza alipokuwa na umri wa miaka mitatu; aliambatana nami kwenye kambi yangu ya mazoezi," amesema Said Mfaume, baba yake Mariam.

Mtanzania huyo mwenye umri wa miaka 38, anayejulikana pia kwa jina la Master Mfaume, ni mkufunzi wa kung fu ambaye anamiliki Klabu ya Kung Fu ya Hekalu la Shaolin ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Anatoa mafunzo ya kung fu kwa vijana 10 wenye umri wa kati ya miaka mitano na 16.

"Tangu alipokuwa na umri wa miaka mitatu hadi sasa, Mariam amekuwa akiendelea vyema na mafunzo ya kung fu," Mfaume, ambaye jina lake la Kichina ni Wang Tianlei, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

"Kung fu iko kwenye damu yangu, na ndoto yangu ni kuwa mkufunzi wa kung fu kama baba yangu katika siku zijazo," Mariam amesema huku akitamka wito wa klabu hiyo ya baba yake, "Kung Fu kwa ajili ya Afya, Kujilinda, na Burudani."

Tangu mwaka 2009, Master Mfaume ametoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 1,500 nchini kote Tanzania, huku sanaa hiyo ya China ikipata umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana katika nchi hiyo.

Amesema kung fu siyo tu inaweza kunufaisha vijana kupitia kujilinda, burudani na kujenga kujiamini, bali pia inatoa ajira kwa kushiriki kwenye uzalishaji wa maudhui ya filamu.

Mwezi Julai, alialikwa kuhudhuria Michezo ya Shaolin 2024 nchini China, iliyofanyika sambamba na mkutano wa kimataifa uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 2,000 kutoka duniani kote.

"Afrika iliwakilishwa na nchi tano, ikiwemo Tanzania, katika Michezo na mkutano wa Shaolin ambapo tulijadili changamoto zinazokabili wakufunzi wa kung fu," amesema, akiongeza kuwa wakufunzi 124 wa kung fu kutoka kote duniani walihudhuria shughuli hiyo.

"Mawasiliano ya kitamaduni kati ya Tanzania na China ni fursa nzuri kwa nchi zote mbili," Mfaume amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha