Lugha Nyingine
Misitu ya kupendeza ya miti kipara ya mivinje katika mji wa Ningguo, mkoa wa Anhui, China yavutia watalii
Wakati msimu wa baridi unapofika, miti katika mbuga ya ardhi oevu ya miti kipara ya mivinje katika kitongoji cha Fangtang, mji wa Ningguo, mkoa wa Anhui, mashariki mwa China imepambwa kwa rangi nyekundu na dhahabu, ikionyesha mandhari ya kupendeza na ya maajabu inayovutia watembeleaji kutoka maeneo ya karibu na mbali.
Mbuga hiyo ya ardhi oevu inajivunia mu zaidi ya 2,000 (kama hekta 133.33) za misitu ya mivinje ya kipara, hali ambayo huunda mwonekano wa kuvutia wa rangi sambamba na mto unaopita katikati ya miti hiyo.
Ikiwa inapatikana kando ya barabara kuu yenye mandhari nzuri ya kusini mwa mkoa huo wa Anhui, mbuga hiyo ni maarufu kipekee kwa majani yake ya msimu wa mpukutiko na baridi. Wakati mzuri wa kuitembelea ni kuanzia katikati ya Novemba hadi mwishoni mwa Desemba, wakati miti ya mivinje iliyozungukwa na maji iko katika kilele cha rangi zake.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma