Kikao cha ufunguzi cha mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwenye kikao cha mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China kwa ajili ya kujadiliwa, inasema China inalenga ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 5 kwa mwaka huu.
Kikao cha ufunguzi cha mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) China imetimiza malengo na majukumu yake makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mwaka 2023, licha ya matatizo na changamoto nyingi kutoka ndani na nje ya nchi, ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwenye kikao cha mkutano wa Bunge la Umma la China kwa ajili ya kujadiliwa imesema.
Mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) umefunguliwa leo Jumatatu saa tisa alasiri katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Rais wa China, na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo.
BEIJING - Bunge la Umma la China (NPC) limefanya mkutano na waandishi wa habari leo siku ya Jumatatu, ikiwa ni siku moja kabla ya ufunguzi wa mkutano wake wa mwaka. Lou Qinjian, msemaji wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China amewaelezea waandishi wa habari kuhusu hali ya mkutano huo uliopangwa kuanzia Machi 5 hadi 11.