Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema mkutano mwingine wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika nchini China mwaka huu, ambapo viongozi wa China na Afrika watakutana tena mjini Beijing baada ya miaka sita kujadili mipango ya ushirikiano wa maendeleo ya siku zijazo na kubadilishana kwa kina uzoefu katika utawala wa nchi.
BEIJING - Viongozi wakuu wa China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wameshiriki kwenye majadiliano ya makundi ya ujumbe wa mikoa mbalimbali ya China kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing siku ya Jumanne. Alipojumuika na wajumbe kutoka Mkoa wa Yunnan katika mjadala wa kikundi, Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, amesisitiza kwamba Yunnan inapaswa kutumia vya kutosha nguvu bora na umaalum wake ili kujiunga vizuri zaidi katika mkakati wa maendeleo yaliyoratibiwa ya sehemu mbalimbali za nchi.
Kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) BEIJING – Mkutano wa Pili wa Bunge la Umma la 14 la China umefunguliwa leo siku ya Jumanne asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, ambapo Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria kikao hicho cha ufunguzi wa mkutano.
Kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing China, Machi 4, 2024. (Xinhua/Rao Aimin) BEIJING - "Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka" ya China, ambayo ni tukio ambalo husubiriwa kwa hamu kubwa kwenye kalenda ya kisiasa ya China, limeanza jana Jumatatu na leo Jumanne kutokana na kufunguliwa kwa mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) na mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, mtawalia huku ikibeba umuhimu mkubwa kwa China na kwingineko duniani.