Lugha Nyingine
Viongozi wa China washiriki kwenye majadiliano ya makundi ya wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China
BEIJING - Viongozi wakuu wa China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wameshiriki kwenye majadiliano ya makundi ya ujumbe wa mikoa mbalimbali ya China kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing siku ya Jumanne.
Alipojumuika na wajumbe kutoka Mkoa wa Yunnan katika mjadala wa kikundi, Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, amesisitiza kwamba Yunnan inapaswa kutumia vya kutosha nguvu bora na umaalum wake ili kujiunga vizuri zaidi katika mkakati wa maendeleo yaliyoratibiwa ya sehemu mbalimbali za nchi.
Akijumuika na wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Sichuan katika majadiliano, Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China ameutaka mkoa huo kutekeleza maamuzi na mipango iliyopangwa na Kamati Kuu ya CPC kwa kutilia maanani hali yake halisi, na kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China alijumuika na wajumbe wa Mkoa wa Guizhou katika majadiliano ametoa wito kwa mkoa huo wa Kusini Magharibi mwa China kutekeleza kwa pande zote maamuzi na mipango iliyopangwa na Kamati Kuu ya CPC, na kufanya kazi kwa bidii kuendeleza maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.
Ding Xuexiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa China alijumuika na wajumbe wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini-Mashariki mwa China kujadili ripoti ya kazi ya serikali. Ding amesisitiza umuhimu wa kutilia maanani kwa karibu kazi kuu ya Chama katika zama mpya kwenye safari mpya na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu ili kupata ufanisi halisi.
Akijumuika na wajumbe wenzake wa Mkoa wa Fujian kujadili ripoti ya kazi ya serikali, Li Xi mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya CPC amesisitiza juhudi za kuendeleza ukaguzi na usimamizi wa nidhamu wa hali ya juu, ili kutoa hakikisho dhabiti la kuijenga China kuwa nchi kubwa na kufikia ustawi wake wa taifa.
Akiongea na wabunge wa Mkoa wa Shandong, Makamu Rais wa China Han Zheng ametoa wito wa utekelezaji wa pande zote wa maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya CPC, na kufanya juhudi zote kuhakikisha maeneo yote ya kazi yanatekelezwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma