超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Viwanda ya roboti za binadamu yapata maendeleo ya kasi na kusukuma mbele uchumi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2024

Kundi la roboti za binadamu zikionyeshwa kwenye lango la maonyesho ya Mkutano wa siku tatu wa Teknolojia za Akili Mnemba Duniani (WAIC) Mwaka 2024 mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Julai 4, 2024. (Xinhua/Fang Zhe)

Kundi la roboti za binadamu zikionyeshwa kwenye lango la maonyesho ya Mkutano wa siku tatu wa Teknolojia za Akili Mnemba Duniani (WAIC) Mwaka 2024 mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Julai 4, 2024. (Xinhua/Fang Zhe)

SHENZHEN – Ndani ya kiwanda cha magari, roboti za binadamu zenye rangi ya fedha zinasonga mbele kwenye mistari ya kuunganisha magari kiwandani, zikifanya kazi ambazo hapo awali zilikuwa zikifanywa na binadamu pekee – kuanzia kwenye uchunguzi wa gari hadi ukaguzi wa mikanda ya kiti na kubandika lebo kwenye magari.

Hili si tukio kutoka kwenye filamu ya hadithi za sayansi, lakini ushirikiano kati ya kampuni ya roboti yenye makao yake mjini Shenzhen UBTECH, na kampuni ya kuunda magari yanayotumia umeme ya NIO ya China, ikionyesha maendeleo ya haraka katika sekta ya roboti binadamu nchini China.

Kadri ushindani unapozidi kuongezeka miongoni mwa watengenezaji, roboti za binadamu zinazidi kujumuishwa katika sekta mbalimbali, huku matumizi ya viwandani yakiongoza.

Mapema mwezi huu, kampuni hiyo ya UBTECH ilitangaza kuwa itafanya kazi na FAW-Volkswagen, mojawapo ya kampuni za kwanza za ubia za China za kuunda magari, ili kuanzisha kiwanda cha magari kisichotumia nguvu kazi ya binadamu.

Mpango huu unalenga kutumia roboti za binadamu za viwandani za UBTECH, Walker S, kwenye kiwanda cha FAW-Volkswagen mjini Qingdao, Mashariki mwa China, ambapo roboti hizo zitafanya kazi kama vile kukaza nati, kuunganisha sehemu za magari, na kushughulikia vipuri vya magari.

Wataalamu wanachukulia uzalishaji viwandani, huduma za biashara, na ukaribu na familia kuwa matumizi ya kimsingi ya roboti za binadamu. Miongoni mwa haya, utengenezaji bidhaa viwandani kwa kutumia roboti hizo utaongoza.

Kwenye Mkutano wa Uvumbuzi Mwaka 2024 uliofanyika Shenzhen, kitovu cha teknolojia na jiji la kisasa kusini mwa China, wikiendi iliyopita, Pang Jianxin, makamu mkuu wa kampuni ya UBTECH, alisema kuwa roboti za binadamu zinazidi kupenya katika sekta muhimu za viwanda vya utengenezaji bidhaa ikiwemo magari, kompyuta, mawasiliano, na vifaa vya matumizi vya kielektroniki.

"Asili sanifu yenye kiwango ya viwanda vya utengenezaji bidhaa inafanya eneo hilo kuwa mwafaka kwa matumizi ya awali ya roboti za binadamu," Pang amesema, akisisitiza kwamba msingi wa viwanda wa China unatoa mazingira mazuri kwa maendeleo ya roboti binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha