超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Kimbunga Gaemi chasababisha mafuriko, uharibifu katika sehemu mbalimbali za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2024
Kimbunga Gaemi chasababisha mafuriko, uharibifu katika sehemu mbalimbali za China
Afisa wa polisi na wafanyakazi wa uokoaji wakimhamisha raia huko Dandong, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Julai 29, 2024. (Xinhua/Long Lei)

FUZHOU/SHENYANG - Kimbunga Gaemi, ambacho ni kimbunga cha tatu kwa mwaka huu kuikumba China, kimesababisha mafuriko na uharibifu katika sehemu mbalimbali za China, ikiwemo mkoa wa mashariki wa Fujian, na mkoa wa kaskazini mashariki wa Liaoning ambapo kimbunga hicho kimeathiri wakaazi 766,900 katika Mkoa wa Fujian, na kusababisha hasara ya moja kwa moja ya kiuchumi inayozidi yuan bilioni 1.6 (dola za Kimarekani karibu milioni 224.35).

Hali hiyo itatathminiwa zaidi, imesema ofisi ya kuzuia na kudhibiti mafuriko ya mkoa huo siku ya Jumatatu, ikiongeza kuwa kwa sasa hakuna ripoti za majeruhi na vifo zilizopokelewa.

Hadi kufikia Jumapili asubuhi, mkoa huo wa Fujian ulikuwa umehamisha watu 312,700 kutoka maeneo hatarishi na kutuma vikosi 2,763 vya uokoaji vinavyojumuisha watu 69,400 na vifaa 15,600, kufanya kazi ya uokoaji wa dharura.

Kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa katika maeneo mengi ya mkoa huo wa Fujian, huku mito 17 ikikumbwa na mafuriko kuanzia Alhamisi hadi Jumapili.

Hitilafu zote za umeme kwenye gridi zilizosababishwa na kimbunga hicho zimetatuliwa, na mtandao wa mawasiliano ya simu unaendelea kuwa thabiti.

Kimbunga Gaemi pia kimeleta mvua kubwa katika mkoa wa Liaoning, kikisababisha viwango vya maji kupanda katika mito 17 na mabwawa zaidi ya 60 katika mkoa wote.

Hadi kufikia saa 1 asubuhi siku ya Jumatatu, wakaazi karibu 60,000 walikuwa wamehamishwa hadi mahali salama, taarifa iliyotolewa na idara ya kudhibiti mafuriko na kukabiliana na ukame ya mkoa huo imesema.

Siku ya Jumatatu asubuhi, idara hiyo ilitoa tahadhari ya rangi ya chungwa kwa Dandong, mji wa mpakani ulioko kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi wa Mto Yalu, na kuinua kiwango cha mwitikio wa dharura kwa mafuriko hadi Ngazi II.

Wakazi zaidi ya 10,000 katika mji huo wa Dandong wamehamishwa kwa usalama.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha