超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Zou Jingyuan ashinda medali ya pili ya dhahabu ya China ya mchezo wa Jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 06, 2024
Zou Jingyuan ashinda medali ya pili ya dhahabu ya China ya mchezo wa Jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris
Zou Jingyuan wa China akishindana kwenye fainali ya jimnastiki za kisanii kwenye milingoti sambamba kwa wachezaji wa kiume katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 mjini Paris, Ufaransa, Agosti 5, 2024. (Xinhua/Lai Xiangdong)

PARIS - Zou Jingyuan alijitahidi kushinda jeraha la bega na kutwaa taji la jimnastiki za kisanii kwenye milingoti sambamba kwa wachezaji wa kiume siku ya Jumatatu na kuipatia China medali ya pili ya dhahabu ya jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris ambapo bingwa huyo mtetezi Zou ni mchezaji pekee wa tatu duniani kushinda medali mbili za dhahabu mfululizo kwenye mashindano ya mchezo huo, akikusanya pointi nyingi 16.200 kumshinda Illia Kovtun wa Ukraine, ambaye alichukua medali ya fedha kwa kupata pointi 15.500.

Shinnosuke Oka wa Japan, bingwa wa jimnastiki ya pande zote, amepata medali ya shaba kwa kujipatia pointi 15.300.

Zou alionekana akiuguza bega lake la kulia baada ya fainali ya jimnastiki ya kujiviringisha na kunyumbua viungo kwa kushikilia pete zenye kuning’inia kwenye kamba mbili siku ya Jumapili, ambapo aliweza kupata medali ya fedha. Alisema baadaye jeraha hilo liliathiri mazoezi yake.

Minyumbuliko ya Zou yenye kukaribia ukamilifu ilivuta hisia kutoka kwa umati kwenye kiwanja cha mashindano cha Bercy. Alikuwa katika udhibiti kamili na kuruka juu ya milingoti kwa miunganisho laini.

Mwenzake Zhang Boheng ambaye ndiyo kwanza ameshinda medali ya fedha ya jimnastiki ya pande zote kwa wanaume amemaliza wa nne katika shindano hilo la Jumatatu.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha