Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Wenyeviti ya mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, akiongoza mkutano wa pili wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 8, 2024. (Xinhua/Wang Ye) BEIJING – Tume ya Wenyeviti ya mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, imefanya mkutano wake wa pili siku Ijumaa ambapo Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo, aliongoza mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine uliamua kuwasilisha nyaraka mbalimbali kwa wajumbe ili kujadiliwa na kupitishwa.
Siku ya Tarehe 8, Machi ilikuwa Siku ya Wanawake Duniani. Katika mikutano mikuu miwili ya China inayoendelea ya Bunge la Umma la China na Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), wajumbe na washauri wa kisiasa wanawake wanafanya kazi muhimu katika kukusanya hekima ili kusukuma mbele maendeleo ya nchi ya China.
BEIJING - Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) Alhamisi lilifanya kikao chake cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wake mkuu wa mwaka, ambapo Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya baraza hilo alihudhuria kikao hicho. Kwenye mkutano huo, wajumbe 14 wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC walitoa maoni yao.
BEIJING - Sera ya China juu ya suala la Taiwan iko wazi, ambayo ni kuendelea kujitahidi kutimiza muungano wa taifa kwa amani kwa dhati mkubwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China. "Jambo la msingi pia liko wazi kabisa: Hatutakubali kamwe Taiwan kujitenga na nchi mama," Wang amesema.