Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akikutana na wafanyakazi wa vyombo vya habari walioripoti habari kuhusu mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, na ametoa salamu na shukrani zake kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2024. (Xinhua/Yao Dawei) BEIJING - Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China amekutana na wafanyakazi wa vyombo vya habari walioripoti habari kuhusu mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, akitoa salamu na shukurani zake siku ya Jumatatu.
Viongozi wa China Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wakihudhuria kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, China, Machi 11, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING – Mkutano mkuu wa mwaka wa Bunge la Umma la 14 la China umefungwa siku ya Jumatatu ambapo viongozi wa China Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kikao cha kufungwa kwa mkutano huo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Watalii kutoka meli ya kitalii ya Zuiderdam wakitembelea eneo la kivutio huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Machi 10, 2024. (Xinhua/Pan Yulong) BEIJING - "Welcome to China!" Waziri wa Utalii na Utamaduni wa China Sun Yeli amesema kwa lugha ya Kiingereza siku ya Jumatatu alipokuwa akifafanua juu ya hatua za kurahisisha safari za kitalii za raia wa kigeni nchini China.
BEIJING - Bunge la Umma la 14 la China limefanya kikao cha kufunga mkutano wake mkuu wa pili wa mwaka leo siku ya Jumatatu kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing ambapo Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria kikao hicho mjini Beijing.